×

Rais Samia Aagana na Viongozi JNIA Kabla ya Safari ya Angola

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan akiagana na viongozi mbalimbali kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Jijini Dar es Salaam kabla ya kuondoka nchini, kuelekea Luanda, Angola ambapo anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika hafla ya Uzinduzi wa Hospitali iliyopewa jina la Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, tarehe 31 Julai, 2026.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, leo Julai 31, 2026, ameondoka nchini kuelekea Luanda, Angola, ambako anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika hafla ya uzinduzi wa Hospitali ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, iliyopewa jina la Baba wa Taifa wa Tanzania.

Kabla ya kuanza safari yake kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar es Salaam, Rais Samia aliagana na viongozi mbalimbali waliofika kumpa heshima na kumuaga.

Aidha, muda mfupi kabla ya kuondoka, Rais Samia alipata fursa ya kuzungumza na Mama Maria Nyerere, mjane wa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, katika mazungumzo yaliyoashiria umuhimu wa tukio hilo la kihistoria na uhusiano wa karibu kati ya Tanzania na Angola.

Rais Dkt. Samia akizungumza na Mama Maria Nyerere muda mfupi kabla ya kuanza safari ya kuelekea Luanda, Angola ambapo anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika hafla ya Uzinduzi wa Hospitali iliyopewa jina la Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, tarehe 31 Julai, 2026.

Leave a Comment