×

Oprah Kufunga Shule Yake ya Wasichana Afrika Kusini Baada ya Miaka 20

Mwanamama maarufu wa vyombo vya habari nchini Marekani, Oprah Winfrey, ametangaza kuwa shule yake ya wasichana nchini Afrika Kusini itafungwa rasmi mwishoni mwa mwaka 2027 baada ya kufanya kazi kwa takribani miaka 20.

Shule hiyo inayojulikana kama Oprah Winfrey Leadership Academy for Girls (OWLAG) ilifunguliwa mwaka 2007 kwa lengo la kutoa elimu kwa wasichana wenye vipaji vya kitaaluma kutoka familia zenye mazingira magumu.

Baada ya kufungwa kwa uendeshaji wake chini ya taasisi ya Oprah, shule hiyo itakabidhiwa kwa serikali ya mkoa wa Gauteng ili iendelee kutoa huduma za elimu kama shule rasmi.

Oprah amesema uamuzi huo utaipa taasisi yake nafasi ya kupanua mpango wa ufadhili wa masomo, hatua ambayo itawawezesha wasichana wengi zaidi nchini Afrika Kusini kupata fursa ya elimu bora.

Kwa takribani miongo miwili, shule hiyo imekuwa ikitambulika kama moja ya miradi mikubwa ya elimu iliyolenga kuwawezesha wasichana wenye vipaji na kuwajengea uwezo wa kuwa viongozi wa baadaye.

Leave a Comment