×

Airtel Money Yazindua “Minyoosho Inaendelea”, Wateja Wapata Nafasi ya Kushinda Zawadi

Dar es Salaam –Airtel Money imezindua rasmi kampeni ya Minyoosho Inaendelea na My Airtel App, yenye lengo la kuwazawadia wateja wanaotumia My Airtel App kufanya miamala yao ya kila siku, huku ikihamasisha Watanzania wengi zaidi kutumia App kufanya miamala bila kikomo kwa urahisi na usalama zaidi.

Minyoosho Inaendelea na My Airtel App ni kampeni ya miezi mitatu inayowapa wateja wote waliopakua na kutumia My Airtel App fursa ya kujishindia zawadi kila wanapofanya miamala kupitia My Airtel App. Baada ya kukamilisha muamala, mteja hupata nafasi ya kuzungusha gurudumu la kidijitali (Spin & Win) na kujishindia zawadi mbalimbali papo hapo.

Kupitia Minyoosho Inaendelea na My Airtel App, mteja anaweza kujishindia zawadi mbalimbali ikiwemo pikipiki, runinga, simu janja, fedha taslimu pamoja na zawadi nyingine nyingi zinazotolewa papo hapo.

Ili kujishindia zawadi kupitia Minyoosho Inaendelea na My Airtel App, mteja anapaswa kufanya miamala mbalimbali kama vile kutuma fedha, kufanya malipo mbalimbali, kununua muda wa maongezi, vifurushi vya intaneti, kulipa bili mbalimbali, kufanya miamala ya kimataifa pamoja na kulipia huduma ya Home Broadband kupitia My Airtel App.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Mkurugenzi wa Airtel Money Tanzania, Andrew Rugamba, alisema kampeni ya Minyoosho Inaendelea na My Airtel App inaonyesha dhamira ya Airtel Money ya kuendelea kuhakikisha kila Mtanzania anafikiwa na huduma za kifedha kidijitali kwa urahisi zaidi.

“Kupitia kampeni yetu ya Minyoosho Inaendelea na My Airtel App, tunataka kuona wateja wetu wanahamasika kutumia Airtel App kufanya miamala yao ya kila siku. Na kila muamala utampa mteja nafasi ya kushinda zawadi papo hapo,” alisema.

Rugamba aliongeza kuwa Airtel ni miongoni mwa kampuni zilizoanzisha matumizi ya mfumo wa michezo ya zawadi katika huduma za kifedha kidijitali (gamification).

“Lengo letu siyo kuwazawadia wateja pekee, bali pia kuwahamasisha Watanzania wengi zaidi kutumia huduma za kifedha kidijitali kupitia My Airtel App na kuchangia kukuza uchumi jumuishi wa kidijitali nchini. Kampeni ya Minyoosho Inaendelea inatoa fursa kwa kila Mtanzania kushiriki katika mfumo wa kifedha wa kidijitali kwa kufanya miamala kwa urahisi na usalama zaidi.aliongeza.

Kampeni ya Minyoosho Inaendelea na My Airtel App inaakisi dira ya ‘Airtel Kila Kona’, inayolenga kusogeza huduma za kidijitali karibu na Watanzania wote, mijini na vijijini, kupitia teknolojia rahisi, bunifu na inayopatikana kwa urahisi.

Tahadhari kuhusu utapeli mitandaoni

Airtel Money inawakumbusha wateja wake wote kuendelea kuwa makini dhidi ya vitendo vya udanganyifu na utapeli wa kifedha, hususan katika kipindi chote cha kampeni.

Washindi wote watapigiwa simu na Airtel  kupitia namba rasmi ya huduma kwa wateja ya Airtel 100 pekee, na pia watapokea ujumbe rasmi wa SMS mara tu wanaposhinda.

Airtel inawasihi wateja wake kutotoa namba zao za siri za Airtel Money (PIN), namba za uthibitisho (OTP), nywila au taarifa zozote binafsi kwa mtu yeyote anayejitambulisha kuwa mfanyakazi wa Airtel kupitia namba nyingine yoyote tofauti na 100.

Airtel Money inawahimiza wateja wote kupakua My Airtel App, kufanya miamala, kuzungusha gurudumu la Spin & Win na kujishindia zawadi mbalimbali zinazotolewa kupitia kampeni ya ‘Minyoosho Inaendelea’, wakati wowote na mahali popote kwa urahisi zaidi.

Leave a Comment