×

Israel Yasimamisha Mpango wa Kutumia Mamba wa Nile Kama Walinzi wa Gereza

Mahakama ya Israel imetoa amri ya muda ya kusimamisha mpango wa kutumia mamba wa mto Nile kama sehemu ya ulinzi kuzunguka gereza linalowashikilia wafungwa wa Kipalestina, baada ya kundi la kutetea haki za wanyama kuwasilisha ombi la dharura la kuzuia utekelezaji wake.

Mpango huo uliokuwa ukiungwa mkono na Waziri wa Usalama wa Taifa wa Israel, Itamar Ben-Gvir, ulihusisha kuchimbwa kwa mtaro maalumu kuzunguka moja ya maeneo ya usalama ya gereza la Ketziot Prison lililopo katika Jangwa la Negev, kisha kuwekwa mamba wa Nile ndani yake.

Maafisa wa Israel walisema hatua hiyo ililenga kuongeza ulinzi na kuzuia uwezekano wa wafungwa kutoroka.

Ripoti zinaeleza kuwa uchimbaji wa mtaro huo ulianza takribani mwezi mmoja uliopita, lakini hadi sasa hakuna mamba ambaye amehamishiwa katika eneo hilo. Mtaro huo ulipangwa kuwa na urefu wa takribani mita 170 na kuzunguka sehemu ya gereza ambako wafungwa wa Kipalestina wanashikiliwa.

Hata hivyo, mpango huo ulizua mjadala mkubwa kutoka kwa mashirika ya haki za binadamu na taasisi za kutetea ustawi wa wanyama, ambazo zilidai kuwa kutumia wanyama wa porini kama sehemu ya ulinzi ni kinyume na kanuni za uhifadhi na ustawi wa wanyama.

Mahakama sasa imeagiza kusitishwa kwa utekelezaji wa mpango huo hadi itakapotoa uamuzi zaidi baada ya kusikiliza hoja za pande zote.

Leave a Comment