Baada ya kuzagaa kwa mijadala mitandaoni inayowalinganisha Wema na Zuchu kabla na baada ya kujifungua, huku baadhi ya watu wakidai kuwa ujauzito wa Wema una utata na hata kudai ulikuwa umetengenezwa kwa teknolojia ya AI (Artificial Intelligence), mmoja wa watu wa karibu na familia ya Wema ameibuka kujibu madai hayo.
Akizungumza na Global TV, ndugu huyo alisema anashangazwa na kiwango cha taarifa zinazosambazwa bila ushahidi, akisisitiza kuwa baadhi ya watu walionekana kutotamani Wema apate mtoto.
Ameeleza kuwa madai yanayodai ujauzito wa Wema ulikuwa wa AI hayana ukweli wowote, akidai ni uzushi unaolenga kupotosha umma na kuichafua familia hiyo.