×

EWURA Yatangaza Bei Mpya za Mafuta, Petroli Yashuka Hadi Sh 3,898 Dar

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imetangaza kushuka kwa bei kikomo za bidhaa za mafuta nchini kuanzia leo, Jumatano, Agosti 5, 2026.

Kwa mujibu wa EWURA:

  • Bei ya petroli imepungua kwa Shilingi 92 kwa lita.
  • Bei ya dizeli imepungua kwa Shilingi 204 kwa lita.
  • Bei ya mafuta ya taa imepungua kwa Shilingi 440 kwa lita.

Kwa mkoa wa Dar es Salaam, bei kikomo ya petroli imepungua kutoka Shilingi 3,990 hadi Shilingi 3,898 kwa lita.

EWURA imewataka wafanyabiashara wote wa mafuta kuzingatia bei kikomo zilizotangazwa na imeonya kuwa hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi ya mfanyabiashara yeyote atakayekiuka maelekezo hayo.

Leave a Comment