×

Wakulima 1,500 Morogoro Wanufaika na Huduma za Mixx by Yas

Zaidi ya wakulima 1,500 mkoani Morogoro wamenufaika na huduma za kifedha kidijitali zinazotolewa na Mixx by Yas kupitia malipo ya stakabadhi za ghala pamoja na mikopo nafuu inayopatikana kupitia jukwaa hilo.

Akizungumza katika Maonesho ya Nanenane yanayoendelea mkoani Morogoro, Meneja wa Biashara wa Mixx by Yas Kanda ya Pwani Kaskazini, Anwar Kisesa, alisema huduma hiyo imewanufaisha wakulima wa mazao mbalimbali ikiwemo ufuta, korosho, mbaazi na kakao kwa kuwawezesha kupokea malipo yao kwa njia salama, ya haraka na rahisi.

Alisema matumizi ya huduma za kifedha kidijitali yanaendelea kuboresha upatikanaji wa huduma za kifedha kwa wakulima, huku yakirahisisha miamala na kuongeza ufanisi katika shughuli za kilimo.

Kisesa alibainisha kuwa Mixx by Yas inaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali wa sekta ya kilimo ili kuwafikia wakulima wengi zaidi kwa huduma za kifedha zitakazowawezesha kukuza uzalishaji na kuchangia maendeleo ya uchumi wa vijijini.

Aidha, aliwahamasisha wananchi wanaotembelea Maonesho ya Nanenane kutumia Mixx Super App kununua tiketi za kuingia viwanjani na tiketi za maegesho ya magari, akisema huduma hiyo husaidia kupunguza foleni na kurahisisha upatikanaji wa huduma katika viwanja vya maonesho.

Leave a Comment