Klabu ya Azam FC leo Agosti 5, 2026, imezindua rasmi jezi zitakazotumika katika msimu wa mashindano wa 2026/27, ikiwa ni sehemu ya maandalizi kuelekea msimu mpya wa mashindano.
Kupitia kurasa zake rasmi za mtandao wa Instagram, klabu hiyo imewaonyesha mashabiki wake muonekano wa jezi hizo mpya kwa kuchapisha picha na video maalum za utambulisho.

Jezi hizo zinatarajiwa kutumika katika mashindano mbalimbali ambayo Azam FC itashiriki msimu ujao, ikiwemo Ligi Kuu ya NBC pamoja kuiwakilisha Tanzania katika Kombe la Shirikisho la CAF.

Kwa sasa, kikosi cha Azam FC kipo nchini Rwanda kikiendelea na kambi ya maandalizi ya msimu mpya (pre-season), ambapo kinafanyia kazi utimamu wa mwili, mbinu za mchezo na kujenga muunganiko wa timu kabla ya kuanza kwa ushindani wa ligi na michuano ya kimataifa.
Azam FC inaingia msimu wa 2026/27 ikiwa na malengo ya kufanya vizuri zaidi ndani na nje ya Tanzania.
