×

Azam FC Yapewa Mpinzani CAFCC, Singida Black Stars Yakutana na Al Ghazala SC

Wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika (CAFCC), Azam FC, wamepangwa kukutana na mshindi kati ya Djibouti Télécom ya Djibouti na ZED FC ya Misri katika raundi ya pili ya awali ya mashindano hayo.

Droo ya CAFCC iliyofanyika leo imeziweka Djibouti Télécom na ZED FC kwenye hatua ya awali, ambapo timu hizo zitachuana kutafuta nafasi ya kusonga mbele. Mshindi wa jumla wa michezo hiyo ataingia raundi ya pili ya awali na kukutana na Azam FC.

Kwa upande mwingine, mwakilishi mwingine wa Tanzania katika CAFCC, Singida Black Stars, amepewa changamoto ya kuanza kampeni yake katika raundi ya kwanza ya hatua ya awali dhidi ya Al Ghazala SC.

Endapo Singida Black Stars itafanikiwa kuvuka hatua hiyo, itakutana na mshindi kati ya Al Ahly FC ya Sudan na Tusker FC ya Kenya katika raundi ya pili ya hatua ya awali.

Timu hizo mbili za Tanzania sasa zinaanza maandalizi ya safari yao ya kuwania mafanikio katika mashindano ya CAF, huku zikilenga kuwakilisha vyema nchi katika michuano ya klabu barani Afrika.

Leave a Comment