×

Video: Chalamila Aagiza Uzio wa Ghorofa Masaki Ubomolewe Papohapo

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, leo Agosti 6, 2026, ameagiza kubomolewa mara moja kwa uzio uliokuwa umezunguuka eneo la ujenzi wa ghorofa huko Masaki, jijini Dar es Salaam.

Hatua hiyo imekuja baada ya kubainika kuwa uzio huo umejengwa ndani ya hifadhi ya barabara ya Toure Drive, kinyume na sheria na kanuni za mipango miji.

Chalamila ametoa maagizo hayo wakati wa ziara yake ya kukagua utekelezaji wa shughuli mbalimbali za maendeleo na hali ya ujenzi katika maeneo ya Masaki.

Amesisitiza umuhimu wa kuzingatia sheria na kanuni za mipango miji ili kuepusha ujenzi holela

Leave a Comment