×

Rais Samia Afanya Mabadiliko, Ateua CEO wa TAFICO na Balozi Malaysia

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amefanya uteuzi wa viongozi wawili katika sekta ya uvuvi na diplomasia, ikiwa ni sehemu ya kuimarisha utendaji wa taasisi za umma na uwakilishi wa nchi nje ya mipaka yake.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Dkt. Moses Kusiluka, Rais Samia amemteua Dkt. Suleiman Peter Kiula kuwa Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Uvuvi Tanzania (TAFICO).

Dkt. Kiula anachukua nafasi ya Bw. Shaibu Ramadhan Matessa, ambaye ameondolewa katika nafasi hiyo na atapangiwa majukumu mengine ya serikali.

Katika uteuzi huo huo, Rais Samia amempangia Balozi Meja Jenerali Mbaraka Naziad Mkeremy kuwa Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Malaysia, ambako ataiwakilisha Tanzania katika masuala ya kidiplomasia na ushirikiano wa kimataifa.

Taarifa ya uteuzi huo imetolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Bakari Machumu, tarehe 6 Agosti 2026.

Leave a Comment