
Bilionea na mwanzilishi wa Amazon, Jeff Bezos, anakaribia kuwa mmoja wa wamiliki wa Liverpool FC, baada ya kuhusishwa na muungano wa wawekezaji unaolenga kununua takribani theluthi moja ya hisa za klabu hiyo.
Kwa mujibu wa taarifa zilizoripotiwa, muungano huo unaongozwa na Amit Bhatia na unatajwa pia kumjumuisha Eduardo Saverin, mwanzilishi mwenza wa Facebook.
Iwapo dili hilo litakamilika, Liverpool itakuwa na thamani ya takribani dola bilioni 6, sawa na karibu TSh trilioni 15.6.
Thamani ya hisa zinazotarajiwa kununuliwa ni takribani dola bilioni 1.8, sawa na karibu TSh trilioni 4.7.
Wamiliki wa sasa wa Liverpool, Fenway Sports Group (FSG), wamethibitisha kuwa wamepokea ombi la uwekezaji kutoka kwa muungano huo, huku mazungumzo yakiendelea.
Dili hilo likikamilika, Bezos ataungana na wawekezaji wengine katika umiliki wa moja ya klabu kubwa na maarufu zaidi katika soka la England.