
Prince William anadaiwa kuwahi kukasirika baada ya King Charles III na Queen Camilla kumtaka mkewe, Kate Middleton, kubadili namna jina lake la kwanza linavyoandikwa kabla ya ndoa yao mwaka 2011.
Kwa mujibu wa mwandishi wa wasifu wa familia ya kifalme, Christopher Andersen, Charles na Camilla walipendekeza jina “Catherine” libadilishwe kuwa “Katherine” ili kuepuka kuongezeka kwa alama za kifalme zinazoanza na herufi C.
Andersen anadai kuwa Charles na Camilla waliona kuwa matumizi ya herufi C katika alama zao za kifalme yangekuwa mengi endapo Kate angeendelea kutumia jina Catherine.

Hata hivyo, ombi hilo lilidaiwa kumkera William, ambaye aliona kuwa si heshima kwa Kate pekee bali pia kwa familia yake. Andersen anaeleza kuwa William alisimama upande wa mkewe na kupinga vikali pendekezo hilo.
Pamoja na hayo, jina hilo halikubadilishwa. Kate aliendelea kutumia Catherine, huku jina lake la kifalme likijulikana rasmi kama Catherine, Princess of Wales.
Andersen pia anasema William amekuwa akimtetea Kate tangu mwanzo wa uhusiano wao, akidai kuwa amekuwa tayari kusimama upande wake katika nyakati mbalimbali za changamoto ndani ya familia ya kifalme.