×

Video: Pinela Atoboa Siri ya Mitoko Yake na Fred Vunjabei, Tetesi Zazimwa!

Mwanadada maarufu mitandaoni, Pinela Justine, amefunguka kuhusu tetesi zinazomhusisha na mfanyabiashara maarufu Bongo, Fred Vunjabei, akikanusha kuwa wawili hao wana uhusiano wa kimapenzi.

Pinela, ambaye pia hujitambulisha kama mwanamitindo na mtumishi wa Mungu, amesema Fred ni bosi wake, mentor na mtu wake wa karibu, akisisitiza kuwa hakuna uhusiano wa kimapenzi unaoendelea kati yao kama ambavyo baadhi ya watu wamekuwa wakidai mitandaoni.

Akizungumzia ukaribu wao, Pinela amesema yeye na Fred wamekuwa wakitoka pamoja katika maeneo mbalimbali kwa ajili ya kujiburudisha na kupata muda mzuri, jambo ambalo limekuwa likiwafanya baadhi ya watu kuanza kuhusisha ukaribu huo na mahusiano ya kimapenzi.

Kauli hiyo imekuja baada ya picha na matukio mbalimbali ya wawili hao kuonekana mitandaoni na kuzua maswali kutoka kwa baadhi ya mashabiki kuhusu aina ya uhusiano uliopo kati yao.

Hata hivyo, Pinela amesisitiza kuwa hakuna kinachoendelea nyuma ya pazia, tofauti na madai yanayosambaa mitandaoni.

Kwa sasa, mwanadada huyo amesisitiza kuwa uhusiano wake na Fred Vunjabei unabaki kuwa wa kikazi, kimalezi na urafiki wa karibu, huku akipuuza madai yanayowahusisha kimapenzi.

Leave a Comment