×

Hichilema Atangazwa Mshindi Uchaguzi wa Urais Zambia

Rais Hakainde Hichilema ametangazwa rasmi mshindi wa uchaguzi wa kiti cha urais wa Zambia  baada ya kupata kura 2,965,326 sawa na asilimia 61 ya kura zilizopigwa katika uchaguzi iliofanyika Agosti 13,2026

Tume ya Uchaguzi ya Zambia (ECZ) imetangaza matokeo ya mwisho kutoka majimbo yote 226, yakionyesha kuwa Hichilema wa chama cha  United Party for National Development amemshinda mpinzani wake mkuu, Brian Mundubile, aliyepata kura 1,856,217 sawa na asilimia 38

 

Ushindi huo unampa Hichilema muhula wa pili wa miaka mitano, baada ya kuvuka kiwango cha zaidi ya asilimia 50 kinachohitajika kushinda uchaguzi katika duru ya kwanza kwa mujibu wa mfumo wa uchaguzi wa Zambia.

Hata hivyo, mchakato wa uchaguzi ulikumbwa na malalamiko baada ya Mundubile kudai kuwepo kwa kasoro katika kujumlisha na kutangaza matokeo, pamoja na madai ya kuingiliwa kwa mchakato huo. Serikali ya Tanzania pia ilikanusha madai ya kuhusika katika uchaguzi huo.

Waangalizi wa uchaguzi wa kikanda na kimataifa walisema siku ya uchaguzi ilikuwa ya amani kwa kiasi kikubwa katika vituo walivyofuatilia. Hichilema sasa anatarajiwa kuanza rasmi muhula wake wa pili kama Rais wa Zambia, huku bado haijabainika iwapo upinzani utapinga matokeo hayo.

Na Ilankize Godfrey

Leave a Comment