×

Rekodi Zambeba Mnyama Simba Dhidi ya Pamba leo

Pamba Jiji FC vs Simba SC ni leo Agosti 19, 2026 Uwanja wa Kirumba rekodi zinambeba mgeni katika mechi 4 ambazo wamekutana licha ya ugumu wa mchezo kila wanapokutana.

Katika mechi 4 zilizopita za ligi safu ya ushambuliaji ya Simba SC imekuwa imara kwa kufunga mabao mengi ikiwa nayo 9 kati ya mabao 12 huku wenyeji Pamba Jiji FC wakifunga mabao 3.

Mnyama amepata ushindi kwenye mechi 3 na sare moja. Hakuna mechi ambayo huwa inakuwa nyepesi dhidi ya Pamba Jiji FC ugenini kutokana na aina ya matokeo yanayopatikana.

Mchezo wa msimu uliopita unaingia katika rekodi inayokumbukwa na mashabiki baada ya Pamba Jiji FC kupata bao la kusawazisha na mwisho matokeo kuwa 1-1.

Haya hapa matokeo ya wababe hawa katika mechi za ligi 22/11/2024, Pamba Jiji FC 0-1 Simba SC,08/05/2025, Simba SC 5-1 Pamba Jiji FC, 19/03/2026, Pamba Jiji FC 1-1 Simba SC na 14/06/2026, Simba SC 2-1 Pamba Jiji FC.

Licha ya rekodi kuwa upande wa Simba SC bado Pamba Jiji FC sio timu nyepesi ikiwa nyumbani ilifungua msimu kwa kutoshana nguvu na Dodoma Jiji FC walipofungana bao 1-1.

Leave a Comment