×

Vieira Apata Kibarua Kipya, Apewa Jukumu la Kuinoa Senegal

 

Gwiji wa zamani wa Arsenal, Patrick Vieira, ametangazwa kuwa kocha mkuu mpya wa timu ya taifa ya Senegal, akichukua nafasi ya Pape Thiaw.

Uteuzi huo umetangazwa rasmi na Shirikisho la Soka la Senegal, Vieira ana uzoefu mkubwa katika soka akiwa mchezaji na kocha.

Mshindi huyo wa Kombe la dunia 1998, anatarajiwa kuingoza Senegal, kuiongoza Senegal katika kampeni za kufuzu AFCON 2027 ambayo Tanzania, Kenya na Uganda zitakuwa wenyeji wa michuano hiyo.

Kwa Vieira, hii inaweza kuwa sura mpya katika safari yake ya ukocha; huku kwa Senegal ikiwa ni mwanzo wa safari yenye matarajio makubwa ya kurejea kwenye kilele cha soka la Afrika.

Baada ya kustaafu kucheza mwaka 2011, Vieira alianza safari yake ya ukocha ndani ya mfumo wa Manchester City, kabla ya kuwa kocha mkuu wa New York City FC mwaka 2016.

Baadaye alifundisha vilabu kadhaa vikiwemo OGC Nice na Strasbourg za Ufaransa , Crystal Palace ya England na Genoa ya Italia.

Senegal imeachana na kocha Thiaw baada ya kutolewa kwenye hatua ya 32 kwa kukubali kichapo cha magoli 3-2 dhidi ya Ubelgiji katika michuano ya Kombe la dunia lilomalizika Marekani mwezi Julai, 2026.

Na Ashura Karimu & Marie Chenda.

Leave a Comment