×

Siri Nzito! Ndege Ya Malaysia Iliyopotea Angani, Haijulikani Ilipoelekea-Video

Tarehe 8 Machi 2014, ndege ya Malaysia Airlines aina ya Boeing 777 iliondoka katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kuala Lumpur kuelekea Beijing, China.

Ndani ya ndege hiyo kulikuwa na watu 239, abiria 227 pamoja na wafanyakazi 12 wa ndege,safari ilianza kawaida, bila taarifa yoyote ya tatizo kubwa. takribani dakika 40 baada ya kuruka, ndege hiyo ilipotea kwenye mifumo ya kawaida ya rada.

Maneno ya mwisho yaliyosikika kutoka kwenye chumba cha marubani yalikuwa “Good night, Malaysian three seven zero.” Kisha mawasiliano yakakatika.

Lakini kilichofuata ndicho kilichoufanya ulimwengu kuanza kujiuliza maswali makubwa.

Transponder ya ndege ilizimwa, na ndege ikaacha kufuata njia yake ya kawaida kuelekea Beijing, badala yake, Boeing 777  ilibadilisha mwelekeo na kuanza kuruka kuelekea magharibi.

Kwa muda mfupi, ndege hiyo iliendelea kuonekana kwenye mifumo ya rada za kijeshi. Hata hivyo, hakuna mawasiliano ya kawaida yaliyokuwa yakipatikana kutoka kwenye ndege .

Swali likawa moja Kwa nini ndege iliyokuwa na watu 239 ilibadilisha njia ghafla na kutoweka bila kutoa tahadhari?

Leave a Comment