
Real Madrid jana usiku Agosti 26, iliibuka na ushindi mnono wa 4-1 dhidi ya Real Sociedad katika mchezo wa La Liga uliopigwa kwenye uwanja wa Santiago Bernabeu, huku Kylian Mbappé akiwa shujaa wa mchezo baada ya kufunga magoli matatu (hat-trick)
Madrid ilianza kwa kasi na Mbappe akifungia bao la kwanza dakika ya 40, baada ya kupokea pasi nzuri kutoka kwa Federico Valverde na kumalizia kwa ustadi.
Hata hivyo, Real Sociedad ilisawazisha kupitia Luka Sučić dakika ya 44, hivyo timu hizo zikaenda mapumziko zikiwa sare ya 1-1.
Kipindi cha pili kilikuwa cha Madrid, Mbappe alifunga bao lake la pili dakika ya 60, baada ya kucheza vizuri na Jude Bellingham ndani ya eneo la hatari na kumalizia kwa shuti la chini.

Dakika 68, Real Madrid iliongeza bao la tatu kupitia Vinícius Júnior, aliyemalizia pasi ya Jude Bellingham na kuifanya Madrid kuongoza 3-1.
Mbappe hakutosheka na mabao mawili, dakika ya 80, Mfaransa huyo alikamilisha hat-trick yake baada ya kupokea pasi nzuri kutoka kwa Vinicius Junior na kumchambua kipa Alex Remiro kwa kumtupia mpira juu yake pia ulikuwa ushindi muhimu kwa Jose Mourinho ambaye amerejea Santiago Bernabeu baada miaka 13.
Mbappe amefikia rekodi ya Gwiji wa zamani wa Los Blancos, Cristiano Ronaldo ya kufunga magoli 86 katika misimu miwili ya kwanza
Ronaldo alifunga mabao 33 katika msimu wa 2009/10 na kisha 53 katika 2010/11, hivyo kufikisha jumla ya mabao 86 baada ya misimu miwili.
Mbappé naye amefanya hivyo hivyo kwa njia tofauti alifunga 44 katika msimu wa 2024/25 na 42 katika 2025/26. Jumla yake mabao 86 pia.
Ronaldo alifikisha mabao 86 katika mechi 89, wakati Mbappé amefikisha kwa mechi 103, Ronaldo alikuwa na asisti 24 dhidi ya 12 za Mbappé katika kipindi hicho, hivyo CR7 bado yupo juu kwa jumla kwa kuchangia magoli 110 dhidi ya 98 za Mbappé.
Na Haika Urio (DaTU)