
Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani umetangaza kifo cha Mtanzania Khalifa H. Siwa, aliyefariki dunia Septemba 2, 2026, katika Jiji la New York, Marekani.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ubalozi wa Tanzania Washington, D.C., Septemba 3, 2026, taarifa hiyo imepokelewa kutoka Ofisi ya Chief Medical Examiner (OCME) ikieleza kuwa Khalifa H. Siwa alifariki baada ya kufanyiwa ajali barabarani katika eneo la Henry Hudson Parkway, North Bound, Jason to 88 Street, New York, 10024.
Taarifa hiyo imeeleza kuwa marehemu alizaliwa Novemba 24, 1972.
Ubalozi umewataka ndugu, jamaa au mtu yeyote anayemfahamu marehemu Khalifa H. Siwa au familia yake nchini Marekani au Tanzania kujitokeza ili kuwasiliana na Ofisi ya OCME, ambayo inahitaji kupata taarifa za “Next of Kin” kwa ajili ya taratibu za kuhifadhi, kumchoma au kusafirisha mwili kwenda Tanzania.
Ubalozi pia umetoa wito kwa mtu yeyote mwenye taarifa zinazoweza kusaidia kuwafikia ndugu wa marehemu kuwasiliana na Richard Lupembe, Afisa Ubalozi, kupitia namba +1 202 468 4441 au barua pepe [email protected].
Ubalozi umesema unathamini ushirikiano wa Watanzania na wadau wote katika kusaidia kufanikisha hatua zinazofuata za utambuzi wa ndugu wa marehemu na taratibu nyingine zinazohusiana na msiba huo.