×

Jason Derulo Aachia Wimbo Mpya “Let Me Be” Akishirikiana Na Qing Madi

Mwanamuziki maarufu wa Pop na R&B kutoka Marekani, Jason Derulo, ameachia rasmi wimbo wake mpya unaoitwa “Let Me Be”, akiwa amemshirikisha msanii chipukizi kutoka Nigeria, Qing Madi, pamoja na The Second Voice.

Derulo ametangaza ujio wa kazi hiyo mpya kupitia ukurasa wake wa Instagram, akiwashirikisha mashabiki wake habari ya kuachiwa kwa wimbo huo.

Ushirikiano kati ya Jason Derulo na Qing Madi unaongeza ladha mpya kwenye kazi hiyo, huku mashabiki wa muziki wakipewa nafasi ya kusikia mchanganyiko wa sauti na mitindo ya wasanii hao.

Qing Madi ni miongoni mwa wasanii chipukizi kutoka Nigeria ambao wameendelea kupata umaarufu katika muziki wa Afrobeat na kuonekana kwenye miradi mbalimbali ya kimataifa.

Kwa upande wake, Jason Derulo ameendelea kujitanua katika muziki wa Pop na R&B kupitia kazi zake pamoja na ushirikiano na wasanii kutoka maeneo mbalimbali duniani.

Wimbo “Let Me Be” tayari umeanza kupatikana kwenye majukwaa mbalimbali ya muziki wa kidijitali, hivyo mashabiki wanaweza kuusikiliza na kuupa sapoti kazi hiyo mpya.

Ujio wa wimbo huo unaendelea kuonyesha namna muziki wa Marekani na Afrika unavyozidi kukutana kupitia ushirikiano wa wasanii kutoka pande hizo mbili.

Stori na Tereza Muga | GPL

Leave a Comment