
Wapo wanaume wengi huwa wakorofi kwa wake zao au wapenzi wao na wanaume wa aina hii wapo wengi. Ukiwa na mwanaume wa aina hii na anakufanyiwa visa mbalimbali na ukorofi ujue kuna kitu labda anataka muachane au ana mchepuko ama ni hulka yake tu kuwa mkorofi.
Visa huwa haviishi sasa unatakiwa ujue jinsi ya kuishi naye; Mfano akianzisha ugomvi wa maneno unashauriwa kumuacha aendelee ili umsaidie kutoa yote ya moyoni wewe kaa kimya usimjibu,tena fanya kama unamsikiliza kwa makini, usiwe mwepesi kujitetea acha amalize yote
kama atakupa muda wa kujieleze muelezee taratibu kwa upendo.
Kama akianzisha mzozo ambao hujui chanzo chake wewe mnyamazie.Akimaliza kelele zake cha kufanya wewe anzisha jambo lingine kabisa mfano mwambie ulimmis sana na umemisi manjonjo yake kitandani tena kimapenzi kabisa ama mwambie muende matembezi au sehemu mliyozoea kwenda pamoja.
DAWA KUBWA YA MWANAUME MKOROFI NI KUWA MNYEYEKEVU.
Hakuna mwanaume mkorofi kwa mwanamke mnyenyekevu hata ungekuwa umemkosea nini ukijishusha ukanyenyekea analainika labda awe na mapepo ndio unyenyekevu wako hautagusa moyo wake.
Mume hafokewi, mume hagombezwi, mume humfanyia jeuri na kiburi, akinuna na wewe unanuna asipokutafuta na wewe humtafuti, utapoteza ndoa yako au upendo.
Kama ni mume wako wa ndoa unaruhusiwa kumng’ang’ania kama ruba, kuwa na tabia ya kumpapatikia mmeo sio kujipendekeza bali ni kuonyesha mapenzi, wewe upo hapo?
Asipokutafuta akitoka nyumbani na kutowasiliana kwa muda mrefu, mtafute, asipoongea na wewe, ongea naye wewe kwa lugha ya mahaba sauti ya mahaba. Kufanya hivyo kutamfanya akupende Zaidi na kukufikiria kila anapokuwa mbali na wewe.
Kunyenyekea hakukugeuzi uonekane bwege, na ukapoteza nafasi yako ya kuwa mke, ila kiburi na jeuri ndio vitakufukuza kwenye hicho kiti na hiyo nafasi ya kuwa mke kuponyoka haraka sana.
Ujeuri weka pembeni! Hivyo ndivyo wanavyofanya waliodumu kwenye ndoa zao. Kwa maelezo haya machache kifupi ni kwamba unyenyekevu kwa mumeo ndio kujenga ndoa yako na ndio dawa pekee na kudumisha ndoa.
Nasisitiza kuwa mnyenyekevu sio kuwa mpumbavu ushauri muhimu ni kwamba panapotakiwa hekima na akili zitumie.
Makala na Elvan Stambuli, Global Digital