×

Yanga Yaondoka Botswana na Sare, Mwalimu Aokoa Jahazi Dakika za Mwisho

Yanga imeanza kampeni ya msimu mpya wa Ligi ya Mabingwa Afrika (CAF Champions League) kwa sare ya 1-1 dhidi ya wenyeji Gaborone United.

Mchezo huo wa mkondo wa kwanza wa hatua ya awali umechezwa katika Uwanja wa Taifa wa Gaborone, Botswana, huku Gaborone United ikianza kwa kupata bao la kuongoza kupitia Obry Amseb dakika ya 33.

Yanga ilijaribu kusaka bao la kusawazisha katika kipindi kilichosalia, lakini ililazimika kusubiri hadi dakika za nyongeza za kipindi cha pili.

Mwalimu aliisawazishia Yanga dakika ya 90+5, na kuifanya timu hiyo ya Tanzania kurejea nyumbani ikiwa na sare muhimu ya 1-1.

Matokeo ya mwisho
Gaborone United 🇧🇼 1-1 🇹🇿 Yanga SC

⚽ 33′ Obry Amseb
⚽ 90+5′ Mwalimu

Matokeo hayo yanaacha kila kitu wazi kuelekea mkondo wa pili, ambapo Yanga itakuwa na nafasi ya kutumia faida ya kucheza mbele ya mashabiki wake kusaka ushindi na tiketi ya kusonga mbele katika mashindano hayo.

Leave a Comment