×

TRA United Yamfukuza Kocha Ndayiragije Baada Ya Mwanzo Mbaya

Klabu ya TRA United SC imethibitisha kufikia makubaliano ya kusitisha mkataba na Kocha Mkuu, Etienne Ndayiragije, kwa makubaliano ya pande zote mbili kuanzia Septemba 7, 2026.

Kupitia taarifa yake, uongozi wa klabu hiyo umemshukuru Ndayiragije kwa mchango wake mkubwa, weledi na huduma aliyotoa kwa timu katika kipindi chote alichokuwa sehemu ya klabu hiyo.

TRA United imemtakia kocha huyo kila la kheri na mafanikio katika hatua inayofuata ya maisha na taaluma yake ya ukocha.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, klabu itaendelea kuwafahamisha wanachama, mashabiki na wadau wake kuhusu hatua zaidi zitakazochukuliwa kuhusiana na uongozi wa benchi la ufundi.

Uamuzi huo unakuja baada ya mwenendo usioridhisha wa TRA United katika michezo mitano ya mwanzo, ambapo timu hiyo imekusanya alama tatu, bila kupata ushindi, ikipoteza michezo miwili na kutoka sare mara tatu.

Leave a Comment