×

YAS Yaendeleza Kampeni Ya Tumaini, Yakabidhi Vifaa Tiba Mbarali

 

Mbarali, Mbeya – Kampuni ya mawasiliano ya Yas Tanzania imeendeleza Kampeni ya Tumaini kwa kukabidhi vifaa tiba pamoja na vifaa vya kujifungulia katika Hospitali ya Wilaya ya Mbarali, Mbeya.

Vifaa hivyo vinatarajiwa kunufaisha wajawazito wanaofika hospitalini hapo kupata huduma, huku msaada huo ukilenga kuongeza upatikanaji wa vifaa muhimu na kusaidia hospitali kutoa huduma bora na salama zaidi kwa mama na mtoto.

Akikabidhi vifaa hivyo, Mkuu wa Yas – Nyanda za Juu Kusini, Frank Protas Antony, alisema Kampeni ya Tumaini ni sehemu ya jitihada za kampuni hiyo za kusaidia jamii, hususan katika maeneo yenye uhitaji.
“Tunataka msaada huu uwe na matokeo ya moja kwa moja kwa wajawazito wanaofika hapa kupata huduma. Kampeni ya Tumaini itaendelea kufikia maeneo mengine nchini,” alisema Antony.

 

Kwa upande wake, mwakilishi wa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali, Dk. Yakub Sanga, aliipongeza Yas Tanzania kwa msaada huo, akisema vifaa vilivyotolewa vitasaidia kuboresha huduma zinazotolewa kwa wajawazito katika hospitali hiyo.

Naye Muuguzi Mkuu, Iman Mwakipusa, pamoja na Kaimu Mganga Mfawidhi, Dk. Albert Sichone, walisema vifaa hivyo vitasaidia kupunguza changamoto ya upatikanaji wa baadhi ya vifaa muhimu vinavyohitajika katika huduma za uzazi.

 

Kampeni ya Tumaini inaendelea kutekelezwa katika maeneo mbalimbali nchini, ikiwa na lengo la kuchangia kuboresha mazingira ya utoaji wa huduma kwa wajawazito na kina mama wanaojifungua.

Hatua hiyo inaendelea kuonyesha umuhimu wa ushirikiano kati ya sekta binafsi na jamii katika kuunga mkono juhudi za kuboresha huduma za afya nchini.

Leave a Comment