×

Makamu wa Rais Aagwa Rasmi na Wizara Ya Nishati Treasury Square, Dodoma

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Deogratias Ndejembi, ameagwa rasmi na Menejimenti ya Wizara ya Nishati pamoja na Taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo katika hafla iliyofanyika katika Ukumbi wa Kambarage, Treasury Square, Dodoma, Jumatano, Septemba 9, 2026.

Hafla hiyo imehudhuriwa na Naibu Waziri wa Nishati, Salome Makamba, Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati anayeshughulikia Umeme na Nishati Jadidifu, Mhandisi Felchesmi Mramba, pamoja na viongozi wa Menejimenti ya Wizara na Wakurugenzi wa Taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo.

Akizungumza katika hafla hiyo, Makamu wa Rais amewaasa viongozi na watendaji hao kuendelea kumuombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, pamoja na wasaidizi wake, ili waendelee kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi na kuwahudumia wananchi.

Aidha, Makamu wa Rais amewataka viongozi na watendaji hao kuendelea kufanya kazi kwa bidii, weledi, uaminifu na uzalendo, akisisitiza kuwa misingi hiyo ni muhimu katika kuhakikisha Serikali inatimiza matarajio ya wananchi.

Amewahimiza pia kuendelea kushirikiana na taasisi mbalimbali za Serikali katika kutekeleza majukumu yao na kuhakikisha sekta ya nishati inaendelea kutoa mchango mkubwa katika maendeleo ya Taifa.

Leave a Comment