Balozi wa China na Viongozi Wengine Wamfariji Rais Samia Kizimkazi Baada ya Kufiwa na Mumewe
Global Publishers September 10, 2026 804 views 0 Comments
SHARE THIS:
Balozi wa China nchini Tanzania, Mhe. Chen Mingjian, akimfariji Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, baada ya kuwasili nyumbani kwake Kizimkazi, Mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar, tarehe 10 Septemba, 2026, kufuatia kufiwa na Mume wake Marehemu Maalim Hafidh Ameir Hassan aliyefariki dunia katika Hospitali ya Kumbukumbu ya Emilio Mzena Zanzibar, tarehe 07 Septemba, 2026.
Viongozi, wanasiasa, mabalozi pamoja na wageni mbalimbali wameendelea kumtembelea na kumfariji Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kufuatia msiba wa Mume wake, Marehemu Maalim Hafidh Ameir Hassan.
Miongoni mwa waliofika kutoa pole ni Balozi wa China nchini Tanzania, Mhe. Chen Mingjian, ambaye amemtembelea Rais Samia nyumbani kwake Kizimkazi, Mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar, leo Septemba 10, 2026.
Aidha, Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, Ndugu Dorothy Semu, pamoja na ujumbe wake, wamefika Kizimkazi kumfariji Rais Samia na familia yake kufuatia msiba huo.
Makatibu Wakuu pamoja na Naibu Makatibu Wakuu nao wamewasili nyumbani kwa Rais Samia kutoa pole na kushiriki katika kipindi hiki cha majonzi.
Marehemu Maalim Hafidh Ameir Hassan alifariki dunia Septemba 7, 2026, katika Hospitali ya Kumbukumbu ya Emilio Mzena, Zanzibar.
Ziara hizo za viongozi na wageni mbalimbali zimeendelea kuwa sehemu ya utaratibu wa kutoa pole kwa Rais Samia na familia yake katika kipindi hiki cha msiba.
Viongozi pamoja na Wageni mbalimbali wakimfariji Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, baada ya kuwasili nyumbani kwake Kizimkazi, Mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar, tarehe 10 Septemba, 2026, kufuatia kufiwa na Mume wake Marehemu Maalim Hafidh Ameir Hassan aliyefariki dunia katika Hospitali ya Kumbukumbu ya Emilio Mzena Zanzibar, tarehe 07 Septemba, 2026.Makatibu Wakuu pamoja na Naibu Makatibu Wakuu wakimfariji Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, baada ya kuwasili nyumbani kwake Kizimkazi, Mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar, tarehe 10 Septemba, 2026, kufuatia kufiwa na Mume wake Marehemu Maalim Hafidh Ameir Hassan aliyefariki dunia katika Hospitali ya Kumbukumbu ya Emilio Mzena Zanzibar, tarehe 07 Septemba, 2026.