×

Diamond na Zuchu Kufanya Sherehe ya Siku 40 ya Mtoto Wao Leo

Familia ya Diamond Platnumz na Zuchu leo, Jumamosi Septemba 12, 2026, inatarajiwa kufanya sherehe ya siku 40 ya mtoto wao wa kike, katika hafla itakayofanyika St. Laurent Garden- Kawe jijini Dar es Salaam.

Diamond Platnumz ametangaza tarehe na eneo la hafla hiyo kupitia mitandao yake ya kijamii, huku tukio hilo likija takribani siku 40 baada ya Zuchu kujifungua mtoto huyo Agosti 2, 2026.

Mtoto huyo ni wa kwanza kwa Zuchu, huku akiwa mtoto wa tano kwa Diamond Platnumz.

Sherehe hiyo inatarajiwa kuwa na mvuto zaidi baada ya watoto wa Diamond na Zari Hassan, Tiffah na Nillan, kuwasili Tanzania wakitokea Afrika Kusini Septemba 9, 2026, kwa ajili ya kushiriki katika tukio hilo la kifamilia.

Kwa sasa, macho ya mashabiki wa Diamond na Zuchu yameelekezwa St. Laurent Garden, ambako familia hiyo inatarajiwa kukutana kusherehekea hatua hiyo muhimu katika maisha ya mtoto wao.

Stori na Razaku Ramadhan | GPL -TUDACO

Leave a Comment