
Kampuni ya Wezesha Mzawa Insurance Broker Limited imetangaza nafasi za kazi kwa Watanzania wenye sifa na uzoefu katika sekta ya bima, mauzo, masoko, biashara, uhasibu na nyanja zinazohusiana.
Nafasi zilizotangazwa ni Business Development Executive, Accountant pamoja na Insurance Sales Executives, huku waombaji wakitakiwa kutimiza vigezo vilivyowekwa kwa kila nafasi.
1. Business Development Executive
Mwombaji anatakiwa kuwa na Shahada ya Kwanza katika Insurance and Risk Management, Sales and Marketing, Business Administration au fani nyingine inayohusiana, pamoja na uzoefu wa angalau miaka miwili katika sekta ya bima, maendeleo ya biashara, mauzo au masoko.
2. Accountant
Mwombaji anatakiwa kuwa na Shahada ya Kwanza katika Accounting au Finance, pamoja na uzoefu wa angalau miaka miwili katika sekta ya bima. Sifa ya CPA ni nyongeza.
3. Insurance Sales Executives
Waombaji wanatakiwa kuwa na Cheti katika Insurance and Risk Management, Sales, Marketing, Business Administration au fani nyingine inayohusiana.
Uzoefu katika sekta ya bima na kazi za mauzo ni nyongeza.
Jinsi ya Kutuma Maombi
Waombaji wanatakiwa kuwasilisha maombi yao pamoja na viambatisho muhimu vilivyothibitishwa kupitia barua pepe au kwa anuani ya ofisi ya kampuni kabla ya Septemba 30, 2026.
Wezesha Mzawa Insurance Broker Limited
P.O. Box 7534, Sinza Mori
Global Group House/Building, Opposite Wanyama Hotel
Dar es Salaam, Tanzania
Barua pepe: [email protected]