×

Mlipuko wa Ebola Wapanuka DRC, Hofu ya Kuvuka Mipaka Yatanda

KINSHASA: Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) imethibitisha kuenea kwa mlipuko wa Ebola hadi eneo jingine nchini humo, hatua inayoongeza hofu ya kusambaa kwa ugonjwa huo katika maeneo zaidi.

Gavana wa jimbo la South Ubangi, kaskazini-magharibi mwa DRC, amesema vipimo vimethibitisha uwepo wa aina ya Ebola ya Bundibugyo, inayohusishwa na mlipuko unaoendelea nchini humo.

Kutokana na hali hiyo, Gavana amewataka wananchi kuchukua tahadhari na kuzingatia hatua za kujikinga dhidi ya ugonjwa huo, ikiwemo kunawa mikono mara kwa mara na kuepuka mikusanyiko ya watu.

Taarifa zinaeleza kuwa mlipuko huo tayari umesababisha vifo vya zaidi ya watu 3,000 nchini DRC.

Wasiwasi mkubwa kwa sasa ni uwezekano wa ugonjwa huo kuvuka mipaka na kuingia katika nchi jirani, kutokana na eneo la South Ubangi kuwa na mipaka na Jamhuri ya Afrika ya Kati pamoja na Jamhuri ya Congo.

Mamlaka zinaendelea kusisitiza umuhimu wa wananchi kuchukua tahadhari na kufuata maelekezo ya wataalamu wa afya ili kupunguza hatari ya maambukizi zaidi.

Leave a Comment