
Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba, leo Septemba 17, 2026, amefanya mazungumzo na Rais wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF), Dkt. Patrice Motsepe, katika Ofisi ya Waziri Mkuu Magogoni, jijini Dar es Salaam.
Mazungumzo hayo ni sehemu ya ziara ya Dkt. Motsepe nchini Tanzania inayolenga kufuatilia maendeleo ya maandalizi ya mashindano ya AFCON 2027, ambayo Tanzania itakuwa mwenyeji kwa pamoja na Kenya na Uganda.
Dkt. Motsepe pia amefanya ukaguzi wa Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam, akifuatilia hatua zilizofikiwa katika maandalizi ya miundombinu kuelekea mashindano hayo.
