×

Corona Yaua Mtu wa Kwanza Burkina Faso

BURKINA FASO imetangaza kifo cha kwanza cha mtu aliyekuwa na ugonjwa wa virusi vya Corona nchini humo, hii ikiwa ni kesi ya kwanza ya kifo kilichotokana na ugonjwa huo kuripotiwa katika eneo la kusini mwa jangwa la Sahara barani Afrika.

 

Profesa Martial Ouedraogo, mkuu wa jopo-kazi la kupambana na virusi vya Corona nchini humo amewaambia waandishi wa habari kuwa aliyeaga dunia kwa Corona ni mwanamke wa miaka 62, aliyekuwa amelazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi.

 

Amesema mwanamke huyo ambaye pia alikuwa anaugua ugonjwa wa kisukari, aliaga dunia usiku wa kuamkia jana Jumatano.

Leave a Comment