×

Rais Mwinyi Amteua Hafsa Mbamba Kuwa Naibu Mkurugenzi ZIPA

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amemteua Hafsa Hassan Mbamba kuwa Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Kukuza Uwekezaji Zanzibar (ZIPA).

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Baraza la Mapinduzi Zanzibar leo, Septemba 18, 2026, uteuzi huo umeanza rasmi tarehe hiyo.

Kabla ya uteuzi huo, Hafsa Mbamba alikuwa Meneja wa Sekta ya Utalii – Taasisi ya Rais, Ufuatiliaji na Usimamizi wa Utendaji Serikalini (PDB).

Hafsa amewahi pia kushika nafasi mbalimbali katika sekta ya utalii Zanzibar, ikiwemo kuwa Katibu Mtendaji wa Tume ya Utalii Zanzibar.

Taarifa hiyo imesainiwa na Mansura M. Kassim, Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi, Zanzibar.

Leave a Comment