×

Bodi ya Wakurugenzi ya Simba Yaunda Kamati ya Uchaguzi

Bodi ya Wakurugenzi ya Simba SC imeunda Kamati ya Uchaguzi itakayoratibu mchakato wa uchaguzi wa klabu hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Bodi hiyo, kikao kilichoketi jijini Dar es Salaam kimeunda kamati hiyo kwa mujibu wa Ibara ya 37 ya Katiba ya Simba ya mwaka 2018.

Kamati hiyo imeundwa na wajumbe watano, ambao ni Boniface Lihamwike anayekuwa Mwenyekiti, Adv. Mwajuma Choggy ambaye ni Makamu Mwenyekiti, pamoja na Richard Mwalibwa, Gerald Mongela na Juma Simba ambao ni wajumbe.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa kamati hiyo itaanza rasmi kazi mara baada ya uteuzi huo.

Taarifa hiyo ilisainiwa na Bodi ya Wakurugenzi ya Simba Sports Club tarehe 26 Novemba 2022.

Leave a Comment