×

TRA Yabaini Utata wa G-Wagon ya Ommy Dimpoz, G350 Yageuka G63

Mercedes-Benz G-Class G350

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imesema imebaini tofauti kubwa kati ya taarifa za forodha na hali halisi ya gari aina ya Mercedes-Benz G-Wagon linalohusishwa na msanii Omary Faraji Nyembo, maarufu kama Ommy Dimpoz. Kwa mujibu wa taarifa ya TRA iliyotolewa, Septemba 28, 2026, gari hilo lilikutwa Septemba 26 katika eneo la Palm Beach Casino jijini Dar es Salaam, likiwa halina namba za usajili, wakati operesheni ya mamlaka hiyo ikiendelea kufuatilia ukwepaji wa kodi za magari.

TRA imesema namba ya utambulisho wa gari hilo (VIN) ni WDB4632762X322756, huku nyaraka za awali za forodha zikilitaja kama Mercedes-Benz G-Class G350 ya mwaka 2020. Hata hivyo, mamlaka hiyo imeeleza kuwa baada ya kufanya uhakiki wa kisayansi na uchunguzi wa Forensic, ilibaini kuwa gari hilo ni Mercedes-Benz AMG G63 ya mwaka 2018.

TRA imeongeza kuwa tofauti hiyo inaashiria uwezekano wa taarifa za gari kuwasilishwa kwa namna ambayo ingeweza kupunguza thamani ya gari katika uthamini wa forodha na hivyo kupunguza kiwango cha kodi kilichopaswa kulipwa.

Leave a Comment