Mama Maria Nyerere Awapa Baraka Washiriki wa Vodacom Nyerere Cycling Tour
Hashpower7113 October 3, 2026 12 views 0 Comments
SHARE THIS:
Wafanyakazi wa Vodacom Tanzania Plc wakiwa katika picha ya pamoja na Mama Maria Nyerere, Madaraka Nyerere, Meneja Mauzo na Mkakati wa Biashara wa Kanda ya Dar es Salaam na Pwani wa Vodacom Tanzania Plc Caleb Majo na Mkuu wa kitengo cha tahadhari wa Stanbic Bank, Wilmot Ishengoma, baada ya hafla ya kuwaaga na kupata baraka kwa waendesha baiskeli wa Nyerere Cycling Tour jijini Dar es Salaam. Safari hiyo kutoka Dar es Salaam hadi Butiama, mkoani Mara, inalenga kumuenzi Baba wa Taifa, hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, kupitia mchezo wa baiskeli na shughuli za maendeleo ya jamii.
Mjane wa Hayati Baba wa Taifa, Julius Nyerere, Mama Maria Nyerere amekutana na waendesha baiskeli wanaoshiriki msafara wa Nyerere Cycling Tour, ambapo amewapa baraka kabla ya kuanza mashindano ya Vodacom Coastal Classic pamoja na safari ya Nyerere Cycling Tour.
Safari hiyo, inayotarajiwa kuanzia Dar es Salaam hadi Butiama, mkoani Mara, inalenga kumuenzi Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, kwa kuunganisha mchezo wa baiskeli na jitihada za kuleta matokeo chanya katika jamii.
Kupitia safari hiyo, waandaaji na washirika wake wanatarajia kutekeleza shughuli mbalimbali katika maeneo ya elimu, afya, uhifadhi wa mazingira, elimu ya fedha na maendeleo ya jamii.
Miongoni mwa shughuli hizo ni utoaji wa madawati 1,000, ujenzi wa madarasa 10, ukarabati wa madarasa 40 pamoja na upandaji miti, huku shughuli hizo zikitarajiwa kuwafikia zaidi ya watu 25,000.
Tukio hilo pia lilihudhuriwa na Meneja Mauzo Mwandamizi wa Vodacom Tanzania Plc, Caleb Majo (kulia), Madaraka Nyerere, mtoto wa Mwalimu Nyerere (wa pili kushoto), na Wilmot Ishengoma, Mkuu wa Kitengo cha Tahadhari wa Stanbic Bank Tanzania (kushoto), pamoja na wadau wengine wa mchezo wa baiskeli.
Tukio hilo lilifanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
Waendesha baiskeli wa msafara wa Nyerere Cycling Tour wakisikiliza wazungumzaji wakati wa kikao cha kuwaaga na kupata baraka kutoka kwa Mama Maria Nyerere kabla ya kuanza mashindano ya Vodacom Coastal Classic pamoja na safari ya Nyerere Cycling Tour kutoka Dar es Salaam hadi Butiama, mkoani Mara. Safari hiyo inalenga kumuenzi Baba wa Taifa, hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, huku ikiunganisha mchezo wa baiskeli na jitihada za kuleta matokeo chanya katika jamii.
Waendesha baiskeli wa msafara wa Nyerere Cycling Tour wakimsikiliza Mama Maria Nyerere akizungumza wakati wa hafla ya kuwaaga na kupata baraka zake kabla ya kuanza mashindano ya Vodacom Coastal Classic pamoja na safari ya Nyerere Cycling Tour kutoka Dar es Salaam hadi Butiama, mkoani Mara. Safari hiyo inalenga kumuenzi Baba wa Taifa, hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, huku ikiunganisha mchezo wa baiskeli na jitihada za kuleta matokeo chanya katika jamii.
Mtoto wa Baba wa Taifa, hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Madaraka Nyerere akizungumza wakati wa hafla ya kuwaaga waendesha baiskeli wa Nyerere Cycling Tour na kutoa salamu za familia ya Mwalimu Nyerere. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam kabla ya kuanza safari ya Nyerere Cycling Tour kuelekea Butiama, mkoani Mara, ikiwa na lengo la kumuenzi Mwalimu Nyerere na kuunganisha mchezo wa baiskeli na jitihada za kuleta matokeo chanya katika jamii.
Meneja Mauzo na mkakati wa biashara wa kanda ya Dar es Salaam na Pwani wa Vodacom Tanzania Plc, Caleb Majo akizungumza na waendesha baiskeli wa Nyerere Cycling Tour wakati wa hafla ya kuwaaga na kupata baraka kutoka kwa Mama Maria Nyerere kabla ya kuanza mashindano ya Vodacom Coastal Classic pamoja na safari ya Nyerere Cycling Tour kutoka Dar es Salaam hadi Butiama, mkoani Mara. Safari hiyo inalenga kumuenzi Baba wa Taifa, hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, kupitia mchezo wa baiskeli na shughuli za maendeleo ya jamii.