
Msanii mkongwe wa Bongo Fleva, Mr. Blue @mrbluebyser1988, amefika ndani ya Studio za Global TV kwa ajili ya mahojiano maalum katika kipindi cha #Kontena.
Katika mahojiano hayo, Mr Blue amezungumzia changamoto zinazoweza kuwakabili vijana, akitoa msisitizo kuhusu namna makundi yanavyoweza kuathiri maisha, kupoteza mwelekeo na kuharibu mipango ya baadaye.