Waziri Mkuu wa Tanzania, Dkt. Mwigulu Nchemba, amezungumza na wawakilishi wa kampuni za SpaceX na Starlink kuhusu uwekezaji wa kampuni hizo nchini katika sekta ya mawasiliano na teknolojia.
Kikao hicho kilifanyika Oktoba 7, 2026, katika Ukumbi wa Hoteli ya Hyatt jijini London, Uingereza, ikiwa ni sehemu ya mazungumzo kuhusu fursa za uwekezaji na maendeleo ya sekta ya teknolojia na mawasiliano nchini Tanzania.

Katika kikao hicho, Waziri Mkuu aliongozana na Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia, Angela Kairuki; Waziri wa Fedha, Balozi Khamis Musa Omar; pamoja na Waziri wa Mipango na Uwekezaji, Kitila Mkumbo.
Mazungumzo hayo yalilenga kuangazia fursa za ushirikiano na uwekezaji katika sekta ya mawasiliano na teknolojia, pamoja na mchango wa teknolojia hizo katika kuimarisha huduma za mawasiliano nchini Tanzania.
