
Waamuzi watakaochezesha mchezo wa watani wa jadi, Simba SC dhidi ya Yanga SC, maarufu kama Kariakoo Derby, wametangazwa kuelekea pambano hilo linalotarajiwa kuchezwa kesho, Oktoba 10, 2026, katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Mchezo huo wa Ligi Kuu ya NBC unatarajiwa kuanza saa 1:00 usiku (19:00), huku macho ya mashabiki wa soka yakielekezwa kwa waamuzi watakaosimamia pambano hilo lenye ushindani mkubwa.
Ahmed Arajiga kutoka Manyara ndiye atakayekuwa mwamuzi wa kati, akisaidiwa na Mohammed Mkono kutoka Tanga na Alli Ramadhan kutoka Zanzibar kama waamuzi wasaidizi.
Alex Panglass kutoka Dar es Salaam atakuwa mwamuzi wa akiba.
Maafisa wengine waliotajwa ni pamoja na Israel Mjuni atakayekuwa mwamuzi msaidizi wa akiba, Mohamed Kaluma kama kamishna wa mchezo, Yahaya Abushehe kama msimamizi wa waamuzi, Fatma Abdallah kama afisa wa waamuzi, Jerry Temu kama afisa wa mechi, Norman Sabuni kama daktari wa mchezo, Maik Warioba kama afisa wa usalama na Said Kipukuswa kama mratibu wa mchezo.
Kwa upande wa timu ya kuripoti kwa mfumo wa FIFA (FVS), watakaohusika ni Leslie Liu nda, Soud Abdi na Charles Ndagala, huku timu ya uendeshaji ikijumuisha Fernando Costa, Ramzi Jebali, Mohamed Kriaa na Tomás Rodrigues.
Simba SC na Yanga SC zinakutana katika moja ya michezo inayosubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wa soka nchini, huku kila upande ukitarajia kupata ushindi dhidi ya mpinzani wake wa jadi.
