
Mwakilishi wa Tanzania katika mashindano ya Miss Grand International 2026, Jihan Mohin Dimachk, anaendelea kuchuana vikali na mwakilishi wa Ecuador, Shyare Andrade, katika kinyang’anyiro cha kuwania taji la Country’s Power of the Year huku mashindano hayo yakitarajiwa kufikia kilele chake kesho, Oktoba 10, 2026.
Hadi sasa, kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa, mwakilishi wa Ecuador anaongoza kwa kupata asilimia 52.28 ya kura, huku Jihan akiwa na asilimia 47.72, hali inayowafanya mashabiki wa Tanzania kuhitajika kuongeza juhudi katika kumpigia kura mwakilishi wao.
Ili Jihan aweze kuongeza kura na kuwa na nafasi ya kutwaa taji hilo, Watanzania na mashabiki wake wanahimizwa kushiriki katika upigaji kura kupitia ukurasa rasmi wa Instagram wa Miss Grand International.

Jihan Dimack, amewaomba Watanzania na mashabiki wake duniani kuendelea kumuunga mkono kwa kumpigia kura ili kutwaa taji la Country’s Power of the Year.
Ili kumuunga mkono, mashabiki wanatakiwa kutembelea ukurasa rasmi wa Instagram wa Miss Grand International kupitia akaunti ya @missgrandinternational, kisha kutafuta chapisho maalumu lenye picha ya Jihan Dimack.
Baada ya kupata chapisho hilo, mashabiki wanatakiwa kufanya mambo yafuatayo:
-
- LIKE: Kupenda chapisho lenye picha ya Jihan.
-
- COMMENT: Kuandika maoni katika chapisho hilo.
-
- REPOST: Kusambaza upya chapisho hilo ili kuwafikia mashabiki wengine.
-
- FOLLOW: Kufuatilia akaunti rasmi ya @missgrandinternational ikiwa bado hawajaifuatilia.

Ushiriki wa mashabiki kupitia mitandao ya kijamii ni sehemu muhimu ya kampeni hii, huku kila mmoja akihamasishwa kuwafikia wengine ili kuongeza uungwaji mkono kwa mwakilishi huyo wa Tanzania.
Jihan amekuwa akipata sapoti kubwa kutoka kwa Watanzania katika hatua zilizopita za mashindano hayo, ambapo alifanikiwa kusonga mbele baada ya kupata kura kutoka kwa mashabiki wake.
Mashindano ya Miss Grand International 2026 yanatarajiwa kufikia kilele chake Oktoba 10, 2026, nchini Thailand, huku mashabiki wa Tanzania wakisubiri kwa hamu matokeo ya safari ya Jihan katika jukwaa hilo la kimataifa.
Kwa Watanzania, ushindi wa Jihan katika kipengele cha Country’s Power of the Year utakuwa fursa ya kuendelea kuitangaza Tanzania kimataifa kupitia mashindano ya urembo.