×

Jihan Atwaa Tuzo ya Global Beauties, Mashabiki Wamiminika Kumpongeza

Miss Grand Tanzania, Jihan Dimack, amepokea pongezi kutoka kwa mashabiki wake baada ya kutangazwa mshindi wa tuzo ya Grand Pageant Choice & Winner kupitia Global Beauties Choices Award, hatua iliyozua furaha miongoni mwa Watanzania na wapenzi wa mashindano ya urembo.

Jihan kupitia ukurasa wake wa Insta @jihandimack, ameeleza furaha na amewashukuru wote wanaondelea kumuunga mkono kwa upendo na sapoti yao.

Kupitia ujumbe wake, Jihan aliandika:

“Asanteni kwa kunichagua kuwa mshindi wa tuzo ya Grand Pageant Choice kupitia Global Beauties Choices Award! Ninajisikia mwenye furaha kubwa, mwenye shukrani na nimebarikiwa sana! Asanteni kwa upendo wenu wote na sapoti mnayoendelea kunipa.” 🥹❤️👑

Ujumbe huo umeibua mashabiki wake, ambao wameendelea kumpongeza na kumtakia mafanikio zaidi katika safari yake ya mashindano ya urembo.

Katika maoni yaliyotolewa kwenye chapisho hilo, mashabiki wengi wameonyesha fahari yao kwa Jihan na kuendelea kuipa Tanzania hamasa ya kufanya vizuri katika mashindano ya kimataifa.

Baadhi ya mashabiki walimweleza kuwa ni mshindi na kumtia moyo kwa maneno kama “You are a winner, born to win,” huku mwingine akimwandikia, “JIHAN, the crown will be yours,” akionyesha matumaini yake kuwa Jihan anaweza kufikia mafanikio makubwa zaidi.

Mashabiki wengine walitumia bendera za Tanzania , emoji za taji 👑 na jumbe za mapenzi kuonyesha sapoti yao kwa mwakilishi huyo wa Tanzania.

Pia, shabiki mmoja kutoka Thailand alionyesha kumuunga mkono Jihan kwa ujumbe wa kumtakia kutwaa taji, ishara ya sapoti inayovuka mipaka ya Tanzania.

Maoni ya mashabiki yanaonyesha namna ambavyo Jihan amekuwa akipata hamasa kutoka kwa watu wanaofuatilia safari yake ya urembo. Hata hivyo, baadhi ya maoni yamehusisha pia mapendekezo kuhusu mwonekano wake, ikiwemo mtindo wa nywele.

Leave a Comment