×

Polisi Dar Wachunguza Kifo cha Mwanamke Mbagala

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam ni Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Muliro Jumanne Muliro

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linachunguza kifo cha mwanamke mmoja mwenye umri unaokadiriwa kuwa kati ya miaka 20 na 25, aliyefariki dunia Oktoba 13, 2026, majira ya saa 11:30 jioni.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Jeshi la Polisi, mwili wa marehemu ulikutwa kwenye bonde lenye uchafu eneo la Kibondemaji, Mbagala, Dar es Salaam, ukiwa umefichwa kichakani.

Taarifa za awali zinaeleza kuwa mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Kituo cha Polisi Mbagala, Temeke, kwa ajili ya hatua zaidi za kisheria.

Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi kubaini chanzo cha kifo hicho na mazingira yaliyopelekea mwanamke huyo kufariki dunia.

Leave a Comment