
Mlimbwende Jihan Dimack amerejea nchini Tanzania kwa mara ya kwanza akiwa Miss Grand International 2026, Oktoba 17, 2026, huku mapokezi yake yakihusisha matukio mbalimbali yaliyoashiria furaha ya kurejea nyumbani.

Jihan Dimack, ambaye amekuwa akiiwakilisha Tanzania katika jukwaa la kimataifa la urembo, amewasili nchini na kupokelewa na watu mbalimbali waliojitokeza kushuhudia kurejea kwake baada ya kushiriki mashindano hayo ya kimataifa.

Mapokezi hayo yamekuwa fursa ya kumpokea mlimbwende huyo na kuonesha mshikamano pamoja na hamasa ya Watanzania katika tasnia ya urembo.
Kurejea kwake nchini kunatarajiwa kuongeza hamasa kwa vijana wanaopenda urembo na kuonesha umuhimu wa kushiriki majukwaa ya kimataifa yanayowapa washiriki nafasi ya kuitangaza Tanzania nje ya mipaka yake.

Matukio mbalimbali katika picha yanaonesha namna Jihandimack alivyorejea nchini katika safari yake ya Miss Grand International 2026.
