
Kwaya ya Mtakatifu Kizito Makuburi, maarufu kama Wazee wa Mimina, nayo haikuwa nyuma katika makamuzi ya kumtukuza Mungu usiku wa Sifa Gospel Fest jijini Dodoma usiku wa kuamkia Oktoba 25, 2026.
Kwaya hiyo imeandika historia kwa kuwa kwaya ya kwanza kutoka Kanisa Katoliki kushiriki tamasha hilo, ikishusha burudani ya aina yake kupitia nyimbo za injili zilizowabeba mashabiki na waumini katika sifa na ibada kwa Mungu.
Kwa umahiri wa uimbaji na namna walivyoliongoza jukwaa, Wazee wa Mimina walithibitisha kuwa muziki wa injili ni daraja muhimu la kuunganisha watu katika kumwabudu Mungu, huku wakiongeza ladha ya kipekee katika tamasha hilo.
Ushiriki wao umeongeza hamasa na kuonyesha namna Sifa Gospel Fest inavyotoa nafasi kwa huduma mbalimbali za muziki wa injili kukutana, kushirikiana na kueneza ujumbe wa Mungu kupitia nyimbo.
Hakika, Dodoma ilipata dozi ya sifa na utukufu wa Mungu kupitia Wazee wa Mimina.