
Simba SC imeibuka na ushindi mwembamba wa bao 1-0 dhidi ya Fountain Gate FC katika mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa Kwaraa, Babati, mkoani Manyara.Bao pekee la mchezo huo limefungwa na beki Rushine De Reuck dakika ya 33, likiipa Simba faida iliyodumu hadi dakika 90 za mchezo zilipokamilika.
Licha ya Fountain Gate kujaribu kupambana ili kurejesha matokeo, vijana hao hawakuweza kupata bao la kusawazisha, huku Simba ikiondoka na pointi tatu muhimu.
Matokeo hayo yanaifanya Simba kuendeleza harakati zake za kutafuta mafanikio katika mashindano ya msimu huu, huku Fountain Gate ikibaki na kazi ya kufanya katika michezo inayofuata.