
Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma (PSRS) imetangaza nafasi nne (4) za kazi katika taasisi mbili za umma ambazo ni Chuo cha Sheria Tanzania (LST) na Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE).
Tangazo hilo lenye kumbukumbu namba Ref. No. JA.9/16/01/62, limetolewa Oktoba 29, 2026, likiwakaribisha Watanzania wenye sifa, uwezo, uadilifu na ari ya kufanya kazi kuomba nafasi hizo.
A. Chuo cha Sheria Tanzania (LST) – Nafasi 3
-
Assistant Lecturer (Conveyancing) – Nafasi 1.
-
Assistant Lecturer (Alternative Dispute Resolution and Quasi Judicial Practice) – Nafasi 1.
-
Assistant Lecturer (Practical Aspects of Commercial Law) – Nafasi 1.
Sifa za waombaji:
-
Awe na Shahada ya Uzamili ya Sheria (Master’s Degree in Law) kutoka taasisi inayotambulika, yenye GPA isiyopungua 3.8.
-
Awe Wakili anayefanya kazi za uwakili kwa kipindi kisichopungua miaka mitano.
-
Awe amehudhuria na kufaulu Postgraduate Diploma in Law katika Chuo cha Sheria Tanzania au kukamilisha programu ya awali ya mafunzo kwa vitendo.
-
Awe na Shahada ya Kwanza ya Sheria yenye GPA isiyopungua 3.5.
Uzoefu katika ufundishaji, tafiti na ushauri wa kitaalamu utakuwa faida ya ziada.
B. Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) – Nafasi 1
4. Assistant Lecturer (Networking) – Nafasi 1.
Sifa za mwombaji:
-
Awe na Shahada ya Uzamili (NTA Level 9) au sifa inayolingana nayo.
-
Awe na Shahada ya Kwanza katika mojawapo ya fani za Computer Science, Information Systems, Information Technology, Computer Engineering, Telecommunication au Electronics.
-
GPA ya Shahada ya Uzamili isiwe chini ya 4.0 au daraja la B+.
-
GPA ya Shahada ya Kwanza isiwe chini ya 3.8.
-
Awe amesomea fani zinazofanana katika ngazi zote mbili za shahada.
Masharti muhimu kwa waombaji
PSRS imeeleza kuwa waombaji wote wanapaswa kuwa raia wa Tanzania na wasiwe na umri unaozidi miaka 45.
Waombaji wanatakiwa kuambatisha nakala zilizothibitishwa za vyeti vya elimu, transcript, vyeti vya usajili wa kitaaluma pale inapohitajika pamoja na cheti cha kuzaliwa.
Pia, kila mwombaji anatakiwa kupakia picha ya Passport Size ya hivi karibuni katika mfumo wa maombi na kutoa majina ya wadhamini watatu (referees) pamoja na mawasiliano yao.
Barua ya maombi iliyosainiwa inapaswa kuandikwa kwa Kiswahili au Kiingereza na kuelekezwa kwa:
Secretary, President’s Office, Public Service Recruitment Secretariat, P.O. Box 2320, Mahakama Street, Tambukareli, Dodoma.
Mwisho wa kutuma maombi
Mwisho: 11 Novemba 2026
Maombi yote yanapaswa kuwasilishwa kupitia mfumo rasmi wa Ajira Portal kwa kutumia anuani ifuatayo >>BONYEZA HAPA
PSRS imesisitiza kuwa maombi yatakayowasilishwa kwa njia nyingine tofauti na mfumo huo hayatakubaliwa.
Aidha, waombaji wanaofanya kazi katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba nafasi hizo, na waombaji waliostaafu katika utumishi wa umma kwa sababu yoyote hawapaswi kutuma maombi.
Ni waombaji watakaopitishwa katika hatua ya awali pekee ndio watakaotaarifiwa kuhusu tarehe ya usaili.
Kwa hiyo, Watanzania wenye sifa zinazotakiwa wanahimizwa kutumia muda uliopo kuandaa nyaraka zao na kutuma maombi kabla ya tarehe ya mwisho.