×

Matokeo ya Darasa la Saba 2026 Yapo Hapa, Asilimia 85.22 Wafulu, Yatangazwa na Necta

Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) limetangaza matokeo ya Mtihani wa Kumaliza Elimu ya Msingi kwa mwaka 2026, huku watahiniwa 970,876 wakifaulu kwa madaraja ya A, B na C, sawa na asilimia 85.22 ya watahiniwa wote waliofanya mtihani huo.

Akitangaza matokeo hayo, Katibu Mtendaji wa NECTA, Profesa Saidi Ally Mohamed, amesema jumla ya watahiniwa 1,139,273 walifanya mtihani huo, huku idadi kubwa ikiweza kupata madaraja yanayowawezesha kuhitimu elimu ya msingi.

Katika hatua nyingine, Profesa Saidi amesema watahiniwa 31 wamefutiwa matokeo kutokana na sababu mbalimbali, zikiwemo ukiukwaji wa kanuni na taratibu za mitihani.

Amefafanua kuwa kati ya watahiniwa hao, 26 wamefutiwa matokeo kwa kufanya udanganyifu wakati wa mtihani, huku wengine watano wakichukuliwa hatua kutokana na kuandika matusi kwenye karatasi za majibu.

Matokeo hayo yanakuja wakati wanafunzi, wazazi na walezi wakisubiri kujua hatua inayofuata ya safari ya elimu kwa wahitimu wa darasa la saba, ikiwemo nafasi za kujiunga na elimu ya sekondari.

BONYEZA HAPA KUTAZAMA MATOKEO >> MATOKEO YA DARASA LA SABA 2026

Leave a Comment