×

Trump Apata Pigo! Democrat Wachukua Seneti na Bunge la Wawakilishi, Mitaa Yafungwa!

Chama cha Democrat kimefanikiwa kupata udhibiti wa Seneti na Baraza la Wawakilishi la Marekani, hatua inayokipa chama hicho ushawishi mkubwa katika Bunge la Congress kwa kipindi kilichosalia cha urais wa Donald Trump.

Ushindi huo umetokana na matokeo ya uchaguzi wa katikati ya muhula (Midterm Elections), ambapo Democrat wamefanikiwa kushinda katika majimbo na maeneo mbalimbali yaliyokuwa yakishikiliwa na chama cha Republican.

Miongoni mwa maeneo yaliyotajwa ni majimbo ya Texas, Kansas na Ohio, ambako wagombea wa Democrat wamepata ushindi katika baadhi ya majimbo ya uchaguzi.

Kwa mujibu wa makadirio ya matokeo yaliyotolewa Democrat inatarajiwa kupata viti 229 katika Bunge la Wawakilishi dhidi ya 164 vya Republican, huku viti 218 vikihitajika ili kupata udhibiti wa chombo hicho cha kutunga sheria.

Katika Seneti, Democrat inatarajiwa kupata viti 54 dhidi ya 43 vya Republican, na hivyo kuvuka idadi ya viti 51 vinavyohitajika kudhibiti chombo hicho. Matokeo hayo yanaonesha Democrat imeongeza viti saba, huku Republican ikipoteza idadi hiyo.

Aidha, katika uchaguzi wa magavana, Democrat imefanikiwa kupata viti 26 na kuongeza viti vinne, huku Republican ikipata viti 19.

Ushindi huo unaashiria mabadiliko makubwa ya nguvu za kisiasa nchini Marekani, huku chama cha Democrat kikitarajiwa kuwa na ushawishi mkubwa katika Bunge la Congress kwa kipindi kilichosalia cha utawala wa Rais Donald Trump.

Wananchama wa Democrat wamefungu mitaa wakiendelea kusherekea ushindi huo.

Leave a Comment