×

Man United Yamtimua Michael Carrick Baada ya Tathmini ya Ndani

Klabu ya Manchester United inadaiwa kufanya uamuzi wa kumfuta kazi kocha Michael Carrick kufuatia tathmini ya ndani iliyofanyika ndani ya saa 48 zilizopita.

Kwa mujibu wa taarifa hizo, uongozi wa klabu hiyo tayari umeafikiana kuhusu hatma ya Carrick, huku kocha huyo akitajwa kupokea taarifa rasmi za kutimuliwa kwake leo.

Uamuzi huo unatajwa kuwa sehemu ya mipango ya Manchester United kufanya mabadiliko katika benchi la ufundi, baada ya viongozi wa klabu hiyo kufanya tathmini ya mwenendo na matokeo ya timu chini ya uongozi wake.

Kuondoka kwa Carrick, iwapo taarifa hizo zitathibitishwa rasmi, kutafungua ukurasa mpya kwa Manchester United katika kipindi ambacho klabu hiyo inahitaji kurejesha ushindani na kuimarisha mwenendo wake ndani na nje ya England.

Hata hivyo, macho sasa yanaelekezwa kwa uongozi wa Manchester United kusubiri tamko rasmi kuhusu hatma ya Carrick pamoja na jina la kocha atakayechukua nafasi yake.

Kwa sasa, klabu hiyo haijatajwa kutoa maelezo rasmi kuhusu sababu za uamuzi huo wala mipango ya mrithi wa Carrick.

Leave a Comment