×

Nandy Atikisa Jukwaa la Tuzo za Malkia wa Nguvu Grand Finale 2026


Staa wa kike wa Bongo Fleva, Faustina Mfinanga almaarufu Nandy usiku wa kuamkia leo Novemba  15, 2026 amewasha moto jukwaani kupitia shoo yake iliyovutia mashabiki katika usiku wa Tuzo za Malkia wa Nguvu Grand Finale 2026, zilizofanyika jijini Dar es Salaam.

Nandy, ambaye ni miongoni mwa wasanii wanaofanya vizuri katika muziki wa Bongo Fleva, ametoa burudani kwa wageni waliohudhuria hafla hiyo iliyolenga kutambua, kuenzi na kuwatuza wanawake waliofanya vizuri katika maeneo mbalimbali ya kijamii na kitaaluma.

Usiku huo umebeba kaulimbiu ya Koleza Levels, ukiwa ni sehemu ya jukwaa la Malkia Wanguvu linalotoa nafasi ya kuwatambua wanawake wenye mchango mkubwa katika jamii na kuwahamasisha wengine kuendelea kupambana na kufikia mafanikio.

Kupitia burudani yake, Nandy ameongeza ladha ya kipekee katika hafla hiyo iliyokusanya wadau mbalimbali, huku shamrashamra za Malkia wa Nguvu 2026 zikiendelea kushuhudia mafanikio na mchango wa wanawake katika jamii.

Leave a Comment